Mji mkuu wa Angola , Luanda umeupiku mji wa Hong Kong na kuwa nafasi ya kwanza ya mji ulio ghali zaidi wa maisha kwa wafanyakazi wataalamu duniani.
Kulingana na uchunguzi wa kila mwaka unaorodhesha viwango vya ughali wa maisha kwa wafanyakazi wataalamu katika miji ya dunia, malipo ya nyumba ya vyumba viwili vya kiwango cha wataalamu mjini Luanda ni dola 4,800 za Kimarekani kwa mwezi, wakati kitafunio cha Hamburger mkahawani ni dola 11 na nusu.
Uchunguzi huo umegundua mji wenye maisha yalio rahisi kwa wafanyakazi wa kigeni ni Tunis nchini Tunisia ukishika nafasi ya 209 na kufuatiwa na mji mkuu wa Kardztan -Bishkek na Skopye Macedonia.
Ni mara ya pili katika kipindi cha miaka mitatu, Luanda unatajwa kuwa mji ghali kabisa kimaisha kuanzia nyumba , usafiri na mavazi , katika orodha ya miji 209 duniani.
