Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mh. Luhaga Mpina ameviagiza vyombo vya dola kuwakamata na kuwashitaki mahakamani mawakala wa makampuni ya ununuzi wa zao la Pamba katika mikoa 15 ya kanda ya magharibi wanaowasambazia wakulima viuatilifu vilivyokwisha muda wake wa matumizi.
Mh. Mpina, ambaye pia ni mbunge wa jimbo la Kisesa katika wilaya ya Meatu mkoani Simiyu, akizungumza na wakulima wa pamba wa vijiji vinne vya kata ya Mwabusalu ambavyo vinatekeleza mradi wa uzalishaji wa mbegu bora ya UKM08, amepiga marufuku tabia ya baadhi ya wakulima kuchanganya mazao mengine kama mahindi na mimea jamii ya mikunde kwenye shamba la pamba.
Hata Akiwa katika kiwanda cha kuchambua pamba kilichojengwa na mwekezaji kampuni ya Gaki Investment tangu mwaka 2012 bila kufanya kazi na hivyo kuminya fursa za ajira kwa wananchi wa jimbo la Kisesa.
Wakulima wa vijiji vya Mwabusalu, Mwakipugila, Ikigijo na Nzanza wamefanikiwa kuzalisha kilo 500 hadi 700 kwa ekari moja kwa kutumia mbegu za UKM08, ukilinganisha na mbegu zilizotumika msimu uliopita wa 2014/2015 za UK91 iliyokuwa ikizalisha wastani wa kilo 200 hadi 300 kwa ekari moja.
