Lukaku alinipiga teke usoni kwa makusudi…

In Kimataifa, Michezo

Beki wa Liverpool Dejan Lovren amemshutumu mshambuliaji wa Manchester United Romelu Lukaku kwa kumpiga teke usoni kwa makusudi katika mechi ya Jumamosi.
Wawili hao walihusika katika mgogoro wa muda mfupi kabla ya kukamilika kwa kipindi cha kwanza katika mechi iliotoka sare ya 0-0 katika uwanja wa Anfield, huku Lovren akisalia amejibiringisha katika uwanja akishikilia uso wake kwa uchungu mwingi.
Mkufunzi wa Liverpool Jurgen Klopp alisema kuwa alidhani kwamba Lukaku alihitaji kupewa kadi nyekundu , lakini hakuna hatua yoyote iliochukuliwa.
”Ukweli ni kwamba alifanya alichokifanya kwa makusudi”, alisema Lovren.”Alikuwa juu yangu na angeondoka tu”.
”Kawaida akifanya hivyo yeye huomba msamaha , lakini nilimuona akiwa amekasirika wakati wa mechi kwa hivyo pengine hiyo ilikuwa sababu”.
Alipoulizwa iwapo hakufurahia kwamba mshambuliaji huyo wa Ubelgiji hatopewa adhabu yoyote , Lovren alijibu.”Huo sio uamuzi wangusiwezi kusema sikufurahia lakini hivyo ndivyo ilivyo”.

Join Our Newsletter!

Get updates, news etc from us. Its simple just put in your email address.

You may also read!

WANAFUNZI 500 WAPEWA MBINU WASILOWEE KWENYE MADAWA YA KULEVYA.

Na Tonie kaisoe ,Arusha Wanafunzi zaidi ya 500 wa shule ya Sekondari Arusha Jiji na Wilaya ya Arumeru wamepewa mbinu

Read More...

MR. IBU AFARIKI DUNIA

Mchekeshaji maarufu wa Nollywood nchini Nigeria, John Okafor, almaarufu Mr. Ibu amefariki dunia baada ya kuugua kwa muda mrefu.

Read More...

POLISI, LATRA WAPIGA FAINI MABASI YALIYO ZIDISHA NAULI ARUSHA.

Jeshi la Polisi kikosi cha Usalama Barabarani Mkoa wa Arusha kwa kushirikaiana na Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini (LATRA)

Read More...

Leave a reply:

Your email address will not be published.

Mobile Sliding Menu