Lukuvi agawa hatimiliki za ardhi 122 kwa wananchi wa Lamadi Mkoani Simiyu.

In Kitaifa
 WAZIRI wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi, amegawa hatimiliki za ardhi 122 kwa wananchi wa Lamadi, mkoani Simiyu wakati alipofanya ziara yake mikoa ya Kanda ya Ziwa, kuhamasisha ulipaji kodi ya pango la ardhi na suala la urasimishaji wa makazi holela.
Wananchi hao 122 ni wale waliofanikiwa kulipia michango yote, hivyo kuondokana na makazi holela na kuishi katika makazi rasmi.
Hata hivyo, jumla ya wananchi 5,200 wa Lamadi Mkoa wa Simiyu wameshapimiwa maeneo yao, kwa urasimishaji, na watapatiwa hati zao mara tu baada ya kukamilisha michango stahili.
Katika ziara hiyo, Waziri Lukuvi alifika Wilaya ya Ilemela mkoani Mwanza, na kufanya ukaguzi wa mfumo wa ulipaji kodi ya pango la ardhi wilayani hapo ,na kugundua kati ya wakazi elfu 35,000 wanaotakiwa kulipa kodi ya ardhi, elfu 28,000 ,wameishapelekewa hati ya madai.
Mbali na hili, Waziri Lukuvi, alitembelea Idara ya Ardhi ya wilayani Nyamagana na kukagua mafaili ya kumbukumbu za wananchi, kuhusu taarifa za ardhi ikiwamo masuala ya hati na kugundua baadhi ya viongozi hawajalipa kodi ya pango la ardhi.

Join Our Newsletter!

Get updates, news etc from us. Its simple just put in your email address.

You may also read!

Viwango vya maadili kwa viongoiz yaongezeka.

Imeelezwa kuwa viwango vya uzingatiwaji wa maadili kwa viongozi na watumishi wa umma nchini,vimeongezeka hadi kufikia asilimi 75.9 kwa

Read More...

Watu 193 wawekwa karantini kisa virusi vya Marburg.

Mganga Mkuu wa serikali Dkt Tumaini Nagu,amesema hakuna kisa kipya kilichoongezeka kuhusu vifo vilivyosababishwa na virusi vya Ugonjwa wa

Read More...

SERIKALI YAFANYA UWEKEZAJI MKUBWA KATIKA HUDUMA ZA HALI YA HEWA

SERIKALI kupitia Wizara ya Ujenzi na uchukuzi,isemema kuwa katika kuhakikisha wanakuwa na Taarifa za uhakika za Hali ya hewa

Read More...

Leave a reply:

Your email address will not be published.

Mobile Sliding Menu