lulu ahukumiwa miaka miwili (2) jela.

In Kitaifa

Mahakama kuu ya Dar es salaam imemhukumu muigizaji wa filamu, Elizabeth Michale, maarufu kama ‘Lulu’, kifungo cha miaka miwili baada ya kumtia hatiani kwa kuua bila kukusudia msanii mwenzake marehemu Steven Kanumba.

Marehemu Steven Kanumba alifariki majira ya saa nane usiku,mnamo mwaka 2012 baada ya kutokea mzozo kati yake yake na Elizabeth Michael ambaye inaaminika kuwa walikuwa na uhusiano wa Kimapenzi.

Mahakama yamhukumu 'Lulu' miak 2 kwa kifo cha Kanumba

Kanumba, ambaye alijizolea umaarufu mkubwa katika ukanda wa Afrika Mashariki na kati na hadi Afrika Magharibi baada ya kuwashirikisha katika filamu zake baadhi ya wasanii maarufu wa kutoka Nigeria akiwemo Mercy Johnson na Noah Ramsey.Marehemu ambaye alizaliwa mwaka 1984, alianza kujipatia umaarufu mwanzoni mwa mwaka 2000 wakati huo akiigiza katika michezo ya runinga kupitia kundi la maigizo la Kaole Sanaa.

Mahakama yamhukumu 'Lulu' miaka 2 jela kwa kifo cha Kanumba

Aliendelea na kuigiza filamu nyingi ambazo zilimpatia umaarufu mkubwa kiasi cha kusafiri mara kadhaa nchi za nje, ambako alitambulika kama mmoja wa wasanii wenye vipaji vikubwa ambaye aliitangaza fani ya filamu nchini Tanzania maarufu kama ‘Bongo Movies.’

Mazishi yake yalichukua sura ya kitaifa kutokana na umaarufu aliojijengea msanii huyo katika jamii ya watanzania na hata nchi za nje.

Join Our Newsletter!

Get updates, news etc from us. Its simple just put in your email address.

You may also read!

JUMLA YA WATU 2249 VISIWA VYA MULEBA WAPATIWA ELIMU YA UGONJWA WA MARBURG .

Baadhi ya Watalaam wa Afya kutoka Wizara ya Afya wakitoa Elimu katika kisiwa Cha Rushonga kilichopo ndani ya ziwa

Read More...

MAANDALIZI DIRA YA MAENDELEO 2050 YAANZA

SERIKALI  imeanza mchakato Wa kuandaa Dira Mpya ya Maendeleo 2050 ambapo wadau wote katika maeneo yao wametakiwa kushiriki kikamilifu

Read More...

Viwango vya maadili kwa viongoiz yaongezeka.

Imeelezwa kuwa viwango vya uzingatiwaji wa maadili kwa viongozi na watumishi wa umma nchini,vimeongezeka hadi kufikia asilimi 75.9 kwa

Read More...

Leave a reply:

Your email address will not be published.

Mobile Sliding Menu