Lwandamina: Uwanja Mbaya Na Hali Ya Hewa Ya Baridi Kali Ilitutesa Sana.

In Kitaifa, Michezo

Kocha mkuu wa Yanga George Lwandamina amesema kwamba timu yake ilishinda kucheza vizuri jana dhidi ya wenyeji, Njombe Mji kwa sababu Uwanja mbaya na hali ya hewa ya baridi kali.
Yanga SC jana wamevuna pointi tatu za kwanza katika Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara baada ya ushindi wa bao 1-0 dhidi ya wenyeji, Njombe Mji Uwanja wa Saba Saba mjini Njombe.

Shukurani kwake, mshambuliaji mpya, Ibrahim Hajib Migomba aliyefunga bao hilo pekee kipindi cha kwanza na sasa Yanga inafikisha pointi nne baada ya kulazimishwa sare ya 1-1 na Lipuli ya Iringa kwenye mchezo wa kwanza nyumbani, Dar es Salaam.

Katika mchezo huo uliochezeshwa na refa Suleiman Kinugani wa Morogoro, aliyesaidiwa na Khalfan Sika wa Pwani na Hajji Mwalukuta wa Tanga, Hajib alifunga bao hilo dakika ya 16 kwa shuti la umbali wa mita 30 la mpira wa adhabu, baada ya yeye mwenyewe kuangushwa.

 

Kocha wa Yanga, George Lwandamina amesema timu yake haikucheza vizuri jana Njombe kwa sababu Uwanja mbaya na baridi kali

Na baada ya mchezo huo, Lwandamina leo amesema kwamba hawakucheza katika kiwango chao kutokana na mazingira ya Uwanja na hali ya hewa, lakini wanashukuru wamechukua pointi tatu.
“Ninamshukuru Mungu tumeshinda, lakini ulikuwa mchezo mgumu sana kutokana na mazingira magumu ya Uwanja wa na hali ya hewa,”alisema.

Join Our Newsletter!

Get updates, news etc from us. Its simple just put in your email address.

You may also read!

Maagizo ya wizara kuhusu mfuko wa maendeleo ya kilimo.

Naibu Waziri Wa Kilimo Anthony Mavunde, amesema serikaliimeanza kutekeleza uanzishwaji wa mfuko wa maendeleo yakilimo utakaosaidia kukabiliana na changamoto

Read More...

TANZIA: WAZIRI MSTAAFU WA KILIMO AFARIKI DUNIA

Aliyewahi kuwa mbunge wa jimbo la Musoma Vijijini na Waziri wa Kilimo na Mifugo Mhe. Herman Kirigini Amefariki Dunia. Akithibitisha

Read More...

Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Professor Makame Mbarawaameliomba Bunge kumuidhinishia kiasi cha Sh Trilioni 3.6ikiwa ni makadirio ya mapato

Read More...

Leave a reply:

Your email address will not be published.

Mobile Sliding Menu