MAADHIMISHO YA WATOTO DUNIANI YAFANYIKA ARUSHA

Siku ya watoto duniani kitaifa imeazimishwa hapa jiji Arusha katika hoteli ya mount meru na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wa serikali na wadau kutoka Tanzania bara na visiwani.

Maadhimisho hayo yenye kauli mbiu isemayo mjengee mtoto uwezo wa kukabiliana na mabadiliko ya tabia ya nchi yameandaliwa UNICEF ,Wizara ya Maendeleo ya jamii jinsia wanawake na makundi maalum,pamoja na ofisi ya Rais Muungano na Mazingira .

Emanuela Kaganda ni mkuu wa wilaya ya Arumeru akitoa salamu kwa niaba ya mkuu wa mkoa wa Arusha John Mongella amesema maadhimisho hayo yataongeza hali ya uelewa wa haki watoto kwa wananchi pamoja na wazazi.

Kwa upande wake mwakilishi mkazi wa shirika la UNICEF Tanzania Ms Elka Wisch amesema kuwa watahakikisha kuwa watoto wanakuwa wanawalinda watoto dhidi ya aina zozote za ukatili.

Amon Mpanju katibu mkuu wizara ya maendeleo ya jamii jinsia wanawake na makundi maalum amesema kuwa kwa Tanzania wameadhimisha siku hiyo November 22 2023 badala ya November 20 kutokana na muingiliano wa majukumu.

Aidha amesema serikali itahakikisha inasimamia haki za watoto dhidi ya ukatili wa aina yeyote ,kuendelezwa kielimu pamoja na kutobaguliwa na jamii.

Kwa upande wake Waziri wa nchi ofisi ya makamu wa Raisi muungano na mazingira Suleiman Jafo upatikanaji wa haki za watoto ni jambo la msingi kwani serikali ya Tanzania imeamua kuwekeza na kuwasaidia watoto katika sekta zote.

Exit mobile version