Maafisa usalama Somalia wafukuzwa kazi.

In Kimataifa

Serikali ya Somalia imewafuta kazi maafisa wawili wa usalama wa ngazi za juu, kufuatia shambulio la mabomu yaliyosababisha mauaji ya watu 27 Jumamosi iliyopita jijini Mogadishu.

Shambulio hilo inaripotiwa kuwa lilitekelezwa na kundi la kigaidi la Al -Shabaab.

Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini humo Abdihakin Dahir Saiid na Mkurugenzi wa Intelijensia Abdillahi Mohamed Sanbaloosh, ndio waliokubwa na adhabu hiyo saa chache baada ya tukio hilo la kigaidi.

Tukio hilo la Jumamosi limeripotiwa ikiwa ni wiki mbili tangu litokee shambulio lingine kubwa zaidi la kigaidi, lililosababisha vifo vya watu 358.

Hata hivyo kundi la Al-Shabaab ambalo linaushirika na kundi la Al-Qaeda, limekanusha kuhusika na tukio la awali huku likikiri kuhusika na tukio la Jumamosi iliyopita

Join Our Newsletter!

Get updates, news etc from us. Its simple just put in your email address.

You may also read!

WANAFUNZI 500 WAPEWA MBINU WASILOWEE KWENYE MADAWA YA KULEVYA.

Na Tonie kaisoe ,Arusha Wanafunzi zaidi ya 500 wa shule ya Sekondari Arusha Jiji na Wilaya ya Arumeru wamepewa mbinu

Read More...

MR. IBU AFARIKI DUNIA

Mchekeshaji maarufu wa Nollywood nchini Nigeria, John Okafor, almaarufu Mr. Ibu amefariki dunia baada ya kuugua kwa muda mrefu.

Read More...

POLISI, LATRA WAPIGA FAINI MABASI YALIYO ZIDISHA NAULI ARUSHA.

Jeshi la Polisi kikosi cha Usalama Barabarani Mkoa wa Arusha kwa kushirikaiana na Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini (LATRA)

Read More...

Leave a reply:

Your email address will not be published.

Mobile Sliding Menu