Maafisa wa Afya nchini Urusi wamesema kuwa,watu zaidi ya 11 wamefariki baada ya upepo mkali kukumba mji mkuu wa nchini hiyo Moscow.

Maafisa wa Afya nchini Urusi wamesema kuwa,watu zaidi ya 11 wamefariki baada ya upepo mkali kukumba mji mkuu wa nchini hiyo Moscow.

Upepo huo mkali uling’oa mamia ya miti, na zaidi ya watu 50 walitafuta matibabu.

Taarifa zinasema nyaya za umeme pia ziliharibiwa, baada ya mvua kubwa iliyoandamana na upepo mkali kukumba mji wa Moscow.

Iwapo idadi hiyo ya waliofariki itathibitishwa, basi itakuwa idadi kubwa zaidi ya watu kuuawa na tufani mjini humo, katika kipindi cha zaidi ya miaka 100.

Exit mobile version