Maafisa wa White House kupewa chanjo ya Corona

Maafisa wa ngazi ya juu katika utawala wa Trump watakuwa miongoni mwa watu wa kwanza watakaopewa chanjo ya corona, maafisa nchini Marekani wamesema.

Maafisa wamesema baadhi ya wafanyakazi wa White House wanatarajiwa kupewa chanjo ya Pfizer/BioNTech wiki hii.

Lakini siku ya Jumapili, Rais Donald Trump alisema chanjo ya mapema itatolewa kwa watu maalumu.

Chanjo hiyo inatoa ulinzi wa hadi asilimia 95 dhidi ya Covid-19 ana inaidhinishwa kuwa salama na wadhibiti wa dawa wa Marekani iliyopita Ijumaa.

Dozi milioni tatu za kwanza za chanjo hiyo kwasaba zinasambazwa katika maeneo tofauti katika majimbo yote 50 ya Marekani.

Exit mobile version