Maafisa wanne wa polisi katika jimbo la Minnesota nchini Marekani wamefutwa
kazi kufuatia kifo cha mtu mwenye asili ya kimarekani weusi, aliyefahamika kwa
jina la George Floyd, ambaye alikuwa amekamatwa na kuonekana akizuiliwa
chini kwa kushikwa shingo. Afisa mkuu wa polisi katika jimbo hilo Medaria
Arradondo amesema kwamba maafisa hao wanne sasa ”sio wafanyakzi wa kikosi
hicho”.
katika video iliosambaa kupitia mtandao wa Instagram inaonesha,George Floyd ,
akilia na kuwaambia maafisa hao weupe ”siwezi kupumua”.
Kisa hicho kinafanana na kile cha Eric Garner, mtu mweusi aliyefariki
akikamatwa na polisi mjini New York mwaka 2014.
Shirika la ujasusi nchini Marekani FBi lilisema litachunguza kisa hicho cha
Minneapolis kilichofanyika Jumatatu jioni.Maafisa wa polisi wa Minnesota
walisema kwamba Floyd mwenye umri wa miaka 46 , ambaye alikuwa anafanya
kazi kama afisa wa usalama katika mkahawa mmoja alifariki akifanyiwa
matibabu kufuatia malumbano na maafisa wa polisi.
Siku ya Jumanne, Meya Jacob Frey alithibitisha kwamba maafisa hao wanne
waliohusishwa na kisa hicho wamefutwa kazi. ”Huu ndio uamuzi
tuliochukua”.Katika mkutano na vyombo vya habari mapema, bwana Frey
alikitaja kisa hicho kama cha kushangaza.
”Ninaamini kwamba kile nilichokiona ni kitendo cha makosa kwa kiwango
chochote kile” , alisema.”Kuwa mtu mweusi nchini Marekani hakustahili kuwa
hukumu ya kifo”.Ni madai ya hivi karubuni ya unyanyasaji unaotekelezwa na
maafisa wa polisi dhidi ya Wamarekani weusi.
Visa maarufu vya hivi karibuni vinashirikisha afisa mmoja wa eneo la Maryland
ambaye alimpiga risasi mtu mmoja akiwa ndani ya gari la kupiga doria.
Kisa hicho cha Minneapolis kilianza baada ya ripoti kwamba mteja mmoja
alikuwa anajaribu kutumia noti bandia ya dola 20 katika duka moja.
Afisa huyo alimuona mshukiwa akiwa ndani ya gari lake, mtu huyo alikataa
kukamatwa kulingana na maafisa wa polisi.
Waliambiwa kwamba mtu huyo ambaye hajata
mbulika alikuwa ameketi juu ya
gari la rangi ya buluu na alionekana kana kwamba ametumia kishawishi fulani.
