Kama utakuwa unakumbuka vizuri siku za nyuma kamanda wa
jeshi la polisi IGP Simon Sirro,aliwataka makamanda wa polisi
kila mkoa kuwa na utaratibu wa kutoa majarida kwa ajili ya
kuelemisha jamii maswala mbali mabali ya kipolisi.
Sasa agizo hilo limepokelewa kwa vitendo na mkoa wa mbeya
ambapo leo kamanada wa polisi mkoani humo Ulrich Matei
amezindua jarida hilo lenye elimu kwa jamii na maelezo ya
shughuli mbali mbali zinazofanywa na jeshi hilo mkoani humo.
