Naibu Waziri Wa Kilimo Anthony Mavunde, amesema serikali
imeanza kutekeleza uanzishwaji wa mfuko wa maendeleo ya
kilimo utakaosaidia kukabiliana na changamoto za wakulima
Nchini.
Naibu Waziri Mavunde ameyasema hayo Bungeni wakati
akijibu swali la nyongeza la Mbunge wa Nanyamba Abdallah
Chikota.
Lakini pia naibu Waziri wa Kilimo Anthony Mavunde amesema
kuwa,Serikali ipo mbioni kuanzisha mfuko wa kukabiliana na
changamoto ya kuporomoka kwa bei ya mazao Nchini katika
mwaka wa fedha 2023/2024.
Naibu Waziri Anthony Mavunde ameyasema hayo wakati
akijibu swali la nyongeza la mbunge wa kiteto Edward Ole
Lekaita aliyehoji kwa nini serikali isinunue alizeti zote za
wakulima ili kunusuru kuporomoka kwa bei licha ya wakulima
kuhamasika kulima zao hilo.
