Waziri wa Maliasili na Utalii Dk Damas Ndumbaro ametoa uamuzi wa kurudiwa kwa mnada kwenye baadhi ya vitalu vya uwindaji kitalii,vilivyobainika kuwa na dosari katika mnada wa sita wa ugawaji vitalu uliofanywa na Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania (TAWA).
Ametoa uamuzi huo wakati akizungumza na waandishi wa habari Jijini Dodoma baada ya kutokea malalamiko kwa baadhi kampuni katika mnada huo.
Amesema katika kampuni ya Bushman Hunting Safari Ltd na Tawa,baada ya kupitia hoja mbalimbali ameamua TAWA kuweka kwenye mnada mara moja kitalu Burko OA kwa kuwa kampuni hiyo iliyoweka dau la Dola za Marekani 400,000 kuomba kujitoa.