SERIKALI imeanza mchakato Wa kuandaa Dira Mpya ya Maendeleo 2050 ambapo wadau wote katika maeneo yao wametakiwa kushiriki kikamilifu katika kutoa mchango wao utakaowezesha kuandaliwa Kwa Dira yenye Maono ya Watanzania Kwa Miaka 25 ijayo.
Amezungumza leo jijini Dodoma kuhusu Hafla ya Uzinduzi Wa mchakato Wa maandalizi ya Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050,naibu katibu Mkuu wizara ya Fedha na Mipango, JENIPHA OMOLO, amesema kuwa ili kufanikisha zoezi la Maandalizi ya Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050 kunategemea Kwa kiasi kikubwa ushiriki Wa wadau wote Kwa Maendeleo ya Taifa na watu wake.
OMOLO,amesema serikali ilifanya tathmini ya utekelezaji Wa Dira 2025 kupitia mikakati na programu za Maendeleo ambapo tathmini hiyo ilibainisha uhitaji Wa Taifa kuanza kupanga vipaumbele vya nchi.
Naibu waziri huyo amesema kuwa ,Uzinduzi Rasmi Wa maandalizi ya Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050 utafanyika tarehe 3 April mwaka huu ambao utafanyika jijini DODOMA ambapo Watanzania wametakiwa kushiriki kikamilifu ili kuwezesha kuwa na Dira ya Watanzania.
