Hospitali ya Taifa ya Muhimbili imepokea wataalamu 16 kutoka nchini Cuba, kama moja ya mikakati yake ya kuboresha utoaji huduma za Afya nchini.
Ikiwa ni pamoja na huduma ya kurekebisha muonekano wa macho ambayo yalipata hitilafu ya kiafya au kutokana na ajali.
Imeelezwa kuwa uwepo wa wataalamu hawa utapunguza wagonjwa kusafirishwa kwenye nje ya nchi, kwa ajili ya matibabu lakini pia utapunguza mrundikano wa wagonjwa wanaosubiri kupatiwa huduma hospitalini.
Hayo yamebainishwa na Dr Mpoki Ulisbisya, ambaye ni katibu mkuu katika wizara ya Afya nchini.
Antenna imenasa sauti ya Dr.Mpoki na hapa anafafanua kuhusiana na hilo.
