Madaktari wametoa sababu ya Wanandoa hawa kufariki wote ndani ya Lisaa Limoja

Kama hukukutana na hii, tunikwambie  inabidi taarifa ikufikie kwamba Jumamosi ya juzi April 22 lilitokea tukio la Kusikitisha lakini la aina yake ambapo Wanandoa Wawili Isaac Vatkin mwenye miaka 91 na mkewe Teressa mwenye miaka 69 Walifariki ndani ya lisaa limoja wakiwa wanapokea matibabu katika hospitali ya Highland Park inayopatikana huko Illinois Chicago.Isaac Vatkin na Teressa enzi za uhai wao wakati wanafunga ndoa

Madaktari wa hospitali hiyo wametoa taarifa kamili kwamba wote walikuwa wanaugua ugonjwa wa Alzheimers, ambapo wote wawili walikuwa wakipata matibabu katika hospitali hiyo na Wao walishangaa pia kuona wanandoa hao wanafariki pamoja.


Wamesema kwamba Teressa ndiye aliyeanza kufariki dunia huku mumewe Vatkin akiwa amemshika mkono akiwa katika kitanda kilichokuwepo jirani na kile alicholala mkewe na kilichowashangaza ni kwamba Mume alivyogundua mkewe amefariki nayeye alifariki dakika 40 baadae.


Hata hivyo wameongeza kwamba kilichopelekea kifo cha Mwanaume huyo ni kushindwa kupumua vizuri lakini kwa upande wa Mtoto wa Marehemu hao aitwaye Clara Gesklinyeye amesema kwamba baba yake asingeweza kuishi bila mkewe kwani walikuwa wanapendana kuliko wanandoa wowote Duniani na anaamini ndio maana baba yao alimfuata mkewe ndani ya dk 40.
“Upendo baina yao ulikuwa mkubwa sana, mmoja asingeweza kuishi bila mwenzake.”
Mtoto huyo amesema hayo wakati anafanya mahojiano na gazeti maarufu ameiambia Daily Mail,

Exit mobile version