Mkuu wa Dawati la Elimu Usalama Barabarani Kamishna
Msaidizi Michael Deleli,ameuagiza uongozi wa Chama cha
Madereva Wasafirishaji Nje ya Tanzania ITDA wafuate sheria
za usalama barabarani ili kudhibiti ajali za barabarani.
Kamishana Michael Deleli ameyasema katika katika zoezi la
uzinduzi wa namba za magari unaolenga kusaidia udhibiti wa
upotevu wa mapato serikalini na kudhibiti vitendo vya uhalifu
hasa kwa madereva wanaosafirisha mizigo kwenda nje ya nchi.
