Madereva wa mabasi yaendayo mkoani,wametakiwa kuendelea
kufuata sheria za usalama bara barani ili kuepuka matukio ya
ajali yanayosababishwa na watumiaji wengine wa vyombo vya
moto
Hayo ya meelezwa na mkuu wa operesheni kikosi cha usalama
bara barani kamishina msaidizi wa polisi ACP Adam Maro,
wakati akizungumza na madereva wa mabasi mkoani Kigoma
na kutaka madereva kuwa viongozi wa kuwaongoza wengine
ambao wamekuwa hawafati sheria za barabarani.
