Madrid yainyoosha Buyern.

 

Klabu ya Real madrid jana imeendeleza ubabe kwa Bayern Munich kwenye mchezo wa nusu fainali ya pili uliochezwa kwenye uwanja wa Santiago Bernabéu. Katika mchezo Huo Madrid imefanikiwa kutinga katika hatua ya fainali japo walitoka suluhu ya kufungana mabao 2-2.

Mabao yote ya Madrid yalifungwa na Karim Benzema (11 na 46) wakati Bayern walipata magoli yao kupitia kwa Joshua Kimmich (3) na James Rodriguez (63).

Real wamefanikiwa kutinga fainali kwa jumla ya mabao 4-3 kutokana na mchezo wa awali uliochezwa wiki iliyopita Allianz Arena. Sasa Madrid anamsubiri mshindi atakayekutana naye fainali katika mchezo utakaochezwa usiku wa leo kati ya AS Roma na Liverpool.

Exit mobile version