MAFURIKO YAUWA 190 MALAWI

Takriban watu 190 sasa wamethibitishwa kufariki nchini Malawi baada ya Dhoruba ya Mafuriko ya Tropiki Freddy kulikumba eneo la kusini mwa Afrika kwa mara ya pili ndani ya mwezi mmoja.

Kiasi cha kutisha cha maji ya kahawia yametiririka katika vitongoji, na kusomba nyumba.

Kitovu cha kibiashara cha Malawi, Blantyre, kimerekodi vifo vingi, 158, wakiwemo 36 katika maeneo ya maporomoko ya ardhi.

Serikali imetangaza hali ya janga katika wilaya 10 za kusini ambazo zimeathiriwa zaidi na dhoruba hiyo.

Wafanyakazi wa uokoaji wamezidiwa, na wanatumia majembe kujaribu kuwatafuta manusura waliofukiwa na udongo.

Shirika la serikali la kusaidia majanga limesema idadi ya waliofariki imeongezeka kutoka 99 siku ya Jumatatu hadi 190, huku takriban watu 584 wakijeruhiwa na 37 bado hawajulikani walipo.

Zaidi ya watu 20,00 wamekimbia makazi yao, iliongeza.

Exit mobile version