Mafuriko Zanzibar yasababisha shule zote kufungwa.

In Kitaifa

shule zote katika kisiwa cha Zanzibar zimefungwa kwa muda kutokana na mvua kali ambayo imesababisha mafuriko.

Waziri wa elimu katika kiswa hicho Riziki Pembe Juma amesema kuwa mvua hiyo ambayo pia imekuwa ikinyesha katika kisiwa cha Unguja na Pemba kwa kipindi cha wiki tatu zilizopita pia imeharibu barabara na mali ya watu.Amesema kuwa baadhi ya shule zimejaa maji hivyobasi kuwa vigumu kwa walimu kufunza mbali na kuwa wanafunzi wanashindwa kufika kutokana na mafuriko.

Waziri huyo amefichua kwamba uamuzi huo uliafikiwa kufuatia pendekezo kutoka kwa kamati ya kukabiliana na majanga ya Zanzibar ambayo iliishauri serikali kufunga shule hizo kwa usalama wa wanafunzi.Baada ya kuangazia mapendekezo hayo tulikuwa hatuna njia nyengine bali kuzifunga shule hadi pale hali itakaporudia hali yake ya kawaida.

Hatahivyo amesema kuwa wanafunzi wa kidato cha sita waliokuwa wakifanya mitihani yao ya mwisho wataendelea kufanya hivyo.

Join Our Newsletter!

Get updates, news etc from us. Its simple just put in your email address.

You may also read!

Serikali kuunga mkono juhudi za Taasisi mbali mbali.

Rais wa Zanzibar Dkt Hussein Mwinyi, amesema serikaliitaendelea kuunga mkono juhudi zinazofanywa na Taasisi yaZanzibar Maisha Bora Foundation,pamoja na

Read More...

DKT. KIRUSWA AZINDUA MFUMO WA USHIRIKISHWAJI WA WATANZANIA KATIKA SEKTA YA MADINI

Watanzania waendelea kunufaika Sekta ya Madini, ajira 15,341 zamwagwa, manunuzi ya ndani ya nchi yafikia Dola za Marekani bilioni

Read More...

MAFURIKO YAUWA 190 MALAWI

Takriban watu 190 sasa wamethibitishwa kufariki nchini Malawi baada ya Dhoruba ya Mafuriko ya Tropiki Freddy kulikumba eneo

Read More...

Leave a reply:

Your email address will not be published.

Mobile Sliding Menu