Mahakama ya hakimu mkazi ya wilayani Mpwapwa mkoani Dodoma imemuhukumu kifungo cha maisha kijana mmoja aliye fahamika kwa jina la Peter Semango almaarufu Madinda mwenye umri wa miaka 23 mkazi wa Kimagai kwa kosa la kumbaka na kumlawiti mdogo wake wa kike mwenye umri wa miaka 8.
Hukumu hiyo imetolewa jana na Hakimu mkazi wa Mahakama hiyo,PASCHAL MAYUMBA baada ya mahakama kujiridhisha bila kuacha shaka lolote kuhusiana na tukio hilo.
Kesi hiyo ilivuta hisia za wasikilizaji na wanaharakati wa haki za mtoto katika Mahakama hiyo.
Akimsomea shitaka hilo mwendesha mashitaka wa polisi GOOD WILL IKEMA amesema mtuhumiwa huyo Alitenda kosa hilo mnamo Juni 13mwaka huu nyumbani kwao mnamo majira ya saa 4 usiku baada ya kumvizia akiwa amelala.
Mwendesha mashitaka huyo amebainisha kuwa kutokana na kijana huyo kufanya kitendo hicho cha ubakaji na ulawiti kwa mdogo wake hivyo anakabiliwa na makosa hayo kinyume na kifungu namba 130kifungu kidogo cha kwanza na cha pili (1 nakifungu cha 131ya kanuni ya adhabu iliyo fanyiwa marejeo mwaka 2002.
Hata hivyo GOODWILL aliiomba Mahakama itoe adhabu kali dhidi ya kijana huyo ili iwe fundisho kwa wengine.
