Mahakama ya Juu ya Venezuela imeshambuliwa na vilipuzi.

In Kimataifa
Mahakama ya Juu nchini Venezuela imeshambuliwa kwa vilipuzi iliyorushwa kutoka  Helikopta ya jeshi la Polisi nchini humo.
Rais Nicolás Maduro amelaani shambulizi hilo lililotokea katika Mahakama hiyo jijini Caracas ni kitendo cha kigaidi na jaribio la kumwondoa madarakani.
Mkanda wa video umeonesha helikopta ya Polisi  ikipaa juu ya jiji hilo kabla ya mlipuko mkubwa kusikika.
Kumekuwa na ripoti kuwa ndege hiyo iliyotumiwa, iliibiwa na rubani ambaye ni afisa wa Polisi.
Polisi huyo amesema serikali ya Maduro ni ya kidhalimu lakini, haijafahamika yuko wapi.
Mahakama hiyo ya Juu imekuwa ikishutumiwa na wanasiasa wa upinzani kwa kutoa maamuzi yanayoegemea rais Maduro.
Licha ya shambulizi hilo, hakuna aliyejeruhiwa ndani na pembezoni mwa Mahakama hiyo.
Tukio hili limekuja wakati huu waandamanaji wa upinzani wakiendeleza shinikizo za kujiuzulu kwa rais Maduro au kufanyika kwa uchaguzi wa mapema.

Join Our Newsletter!

Get updates, news etc from us. Its simple just put in your email address.

You may also read!

PROF. NDALICHAKO AKIPONGEZA KIWANDA CHA MBOLEA CHA ITRACOM KWA UTEKELEZAJI SHERIA ZA KAZI

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Prof. Joyce Ndalichako amekipongeza kiwanda

Read More...

WATOTO 109,514 KUPATIWA CHANJO YA MATONE DHIDI YA POLIO WILAYANI NKASI MKOANI RUKWA

Katika utekelezaji wa zoezi la Kampeni ya chanjo ya matone dhidi ya ugonjwa wa  Polio, Halmashauri ya Wilaya ya Nkasi

Read More...

Tigo na mjasiriamali Boss yaja kukomboa wajasiriamali

Katika kuendelea kukuza utalii wa utamaduni hapa nchini kampuni ya Tigo kanda ya kaskazini imeendeleaa kuwaunga mkono wadau wa

Read More...

Leave a reply:

Your email address will not be published.

Mobile Sliding Menu