Mahakama ya Uhalifu ya Kimataifa ya The Hague, Uholanzi, mwezi ujao itaamua kama Afrika Kusini ilikiuka sheria za kimataifa pale iliposhindwa kumtia mbaroni Rais Omar al-Bashir alipotembelea taifa hilo 2015.
Serikali ya Afrika Kusini na mahakama hiyo ziliingia katika mvutano mkali wakati Bashir aliporuhusiwa kuhudhuria mkutano wa kilele wa Umoja wa Afrika mjini Johannesburg pamoja na mahakama ya ICC kutoa waranti mbili za kukamatwa kwa kiongozi huyo.
Wanasheria wa Afrika Kusini wanadai serikali ilishauriana na majaji wa ICC kabla ya mkutano wa kilele na ikakubalika anaweza kuwa na kinga ya kidiplomasia kama mkuu wa nchi.
Rais Bashir bado anaendelea na majukumu yake pamoja na kusakwa kwa tuhuma ya mauwaji ya halaiki yalotokea katika jimbo la Darful nchini Sudan.
