Mahakama ya Wilaya ya Mlele mkoani Katavi, imewahukumu kifungo cha jumla ya miaka 60 jela washtakiwa watatu, kwa kukutwa na mguu wa twiga kinyume cha sheria za wanyama pori.
Hukumu hiyo imetolewa na Hakimu Mkazi Mfawidhi wa mahakama hiyo Teotimus Swai, baada ya kuridhishwa na ushahidi uliotolewa na upande wa mashtaka.
Akitoa hukumu hiyo hakimu Swai amesema kuwa, ushahidi uliotolewa mahakamani na upande mashtaka umewatia hatiani watuhumiwa hao.
Waliohukumiwa kwenda jela ni Juma Kinanda (66) na Saidi Shabani (42), wote wakazi wa Wilaya ya Sikonge mkoani Tabora na Rashidi Miraji (64) mkazi wa Inyonga wilayani Mlele.
