Mahakama yaondoa marufuku ya maandamano Kenya.

In Kimataifa

Mahakama kuu nchini kenya imeondoa kwa muda marufuku kwa maandamano dhidi ya tume ya uchaguzi ya chi hiyo IEBC.
Muungano wa upinzani (Nasa) ulikuwa tayari umetangaza kuwa hingefanya maandamano leo dhidi ya tume ya uchaguzi, ili kuwaruhusu viongozi wake kuwatembelea watu walipigwa na polisi wakati wa maandamano.
Katika taarifa, msemaji wa kiongozi wa Nasa, Raila Odinga, Dennis Onyango, alisema kuwa watasitisha maandamano leo kuonyesha huruma kwa wale waliojeruhiwa na polisi wakati wa maandamano.
Nasa imewalaumu polisi kwa kutumia nguvu nyingi dhidi ya waandamanaji, madai ambao polisi wamekana.
Mwanafunzi aliuawa kwa kupigwa risasi siku ya Jumatatu wakati wa maandamano mjini Kisumu, magharibi mwa Kenya.
Maandamano yalizuka baada ya uchaguzi wa mwezi Agosti, ulioshindwa na Rais Uhuru Kenyatta.
Mahakama ya juu zaidi iliamua kuwa uchaguzi huo ulikuwa na hitilafu.
Bw. Odinga anasema hatashiriki marudio ya uchaguzi wa wiki ijayo kwa sababu matakwa yake kwa tume ya uchaguzi kufanyiwa mabadiliko hayajatekelezwa.

Join Our Newsletter!

Get updates, news etc from us. Its simple just put in your email address.

You may also read!

WANAFUNZI 500 WAPEWA MBINU WASILOWEE KWENYE MADAWA YA KULEVYA.

Na Tonie kaisoe ,Arusha Wanafunzi zaidi ya 500 wa shule ya Sekondari Arusha Jiji na Wilaya ya Arumeru wamepewa mbinu

Read More...

MR. IBU AFARIKI DUNIA

Mchekeshaji maarufu wa Nollywood nchini Nigeria, John Okafor, almaarufu Mr. Ibu amefariki dunia baada ya kuugua kwa muda mrefu.

Read More...

POLISI, LATRA WAPIGA FAINI MABASI YALIYO ZIDISHA NAULI ARUSHA.

Jeshi la Polisi kikosi cha Usalama Barabarani Mkoa wa Arusha kwa kushirikaiana na Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini (LATRA)

Read More...

Leave a reply:

Your email address will not be published.

Mobile Sliding Menu