Mahakama yaruhusu duru ya pili ya uchaguzi wa rais Liberia.

In Kimataifa

Mahakama kuu ya Liberia imesema kuwa ushahidi wa vitendo visivyokubalika katika uchaguzi wa Rais duru ya kwanza mwezi Oktoba hautoshi kuufanya uchaguzi kurudiwa.

Hii inamaanisha kuwa mzunguko wa mwisho wa uchaguzi kati ya wagombea wawili waliokuwa wakiongoza yaani George Weah na Makamu wa Rais Joseph Boakai unaruhusiwa kuendelea.

Sasa inasubiriwa tume ya uchaguzi kuweka na kuitangaza siku ya kupiga kura.

Mwakilishi wa chama cha Liberty Charles Brumskine ambaye alikuwa katika nafasi ya tatu katika mzunguko wa kwanza alikuwa ameyapinga matokeo akitaka uchaguzi urudiwe.

Mzunguko wa pili wa kumchagua mrithi wa rais Ellen Johnson Sirleaf awali ulikuwa umepangwa kufanyika mwezi uliopita, Novemba.

Liberia ambayo ni nchi iliyoundwa na watumwa walioachiwa huru huko Marekani katika karne ya 19, haijawahi kuwa na makabidhiano ya madaraka kawa miaka 73.

Bi Sirleaf alitwaa urais mwaka 2006 baada ya mwaka 2003 waasi kumwondoa kwa lazima kiongozi wa wakati huo Charles Taylor, tukio hilo likikomesha vita vya wenyewe kwa wenyewe vilivyodumu kwa miaka mingi.

Hivi sasa Taylor anahudumia kifungo cha miaka 50 jela nchini Uingereza kutokana na makosa yanayohusiana na majirani zao Sierra Leone.

Join Our Newsletter!

Get updates, news etc from us. Its simple just put in your email address.

You may also read!

Maagizo ya wizara kuhusu mfuko wa maendeleo ya kilimo.

Naibu Waziri Wa Kilimo Anthony Mavunde, amesema serikaliimeanza kutekeleza uanzishwaji wa mfuko wa maendeleo yakilimo utakaosaidia kukabiliana na changamoto

Read More...

TANZIA: WAZIRI MSTAAFU WA KILIMO AFARIKI DUNIA

Aliyewahi kuwa mbunge wa jimbo la Musoma Vijijini na Waziri wa Kilimo na Mifugo Mhe. Herman Kirigini Amefariki Dunia. Akithibitisha

Read More...

Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Professor Makame Mbarawaameliomba Bunge kumuidhinishia kiasi cha Sh Trilioni 3.6ikiwa ni makadirio ya mapato

Read More...

Leave a reply:

Your email address will not be published.

Mobile Sliding Menu