Wabunge 8 wa viti maalum wa chama cha wananchi CUF waliofukuzwa uanachama na kupoteza nafasi zao, wanakabiliwa na mtihani mgumu baada ya mahakama kutupilia mbali ombi lao.
Wabunge hao waliitaka Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam, kuweka zuio la kuapishwa kwa wabunge wapya, walioteuliwa katika nafasi hizo.
Badala yake mahakama hiyo imesema itatoa uamuzi wa pingamizi la Mwanasheria Mkuu wa Serikali AG, dhidi ya maombi ya wabunge hao na madiwani wawili, wanaopinga kufukuzwa uanachama Agosti 25 mwaka huu.
Uamuzi huo umetolewa jana na Jaji Lugano Mwandambo, baada ya kusikiliza hoja za pande zote mbili.
