Makame Mbarawa amempa muda wa miezi kumi Mkandarasi wa Kampuni ya CICO kukamilisha ujenzi wa bara bara.

In Kitaifa
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa amempa muda wa miezi kumi Mkandarasi wa Kampuni ya CICO anayejenga barabara ya Tabora-Sikonge yenye urefu wa km 30 kwa kiwango cha lami kukamilisha kazi hiyo.
Mbarawa ameyasema hayo mkoani Tabora mara baada ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa barabara hiyo na kuelezea kutoridhishwa na kasi ya ujenzi wake.
Ameongeza kuwa ukamilishaji wa barabara hiyo uendane na viwango na ubora vinavyoendana na thamani ya fedha waliyopewa, ili barabara hiyo iweze kudumu kwa muda uliopangwa.
Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Tabora Mjiini Mwalimu Queen Mlozi, amemshukuru Prof. Mbarawa kwa kufuatilia kwa karibu mradi huo ambao utachochea kasi ya maendeleo mkoani humo.
Naye, Meneja wa Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS), mkoa wa Tabora Eng. Damian Ndabalinze, amemhakikishia Prof. Mbarawa kuwa atamsimamia mkandarasi huyo kikamilifu ili barabara hiyo ikamilike katika kipindi cha miezi kumi.

Join Our Newsletter!

Get updates, news etc from us. Its simple just put in your email address.

You may also read!

Serikali kuunga mkono juhudi za Taasisi mbali mbali.

Rais wa Zanzibar Dkt Hussein Mwinyi, amesema serikaliitaendelea kuunga mkono juhudi zinazofanywa na Taasisi yaZanzibar Maisha Bora Foundation,pamoja na

Read More...

DKT. KIRUSWA AZINDUA MFUMO WA USHIRIKISHWAJI WA WATANZANIA KATIKA SEKTA YA MADINI

Watanzania waendelea kunufaika Sekta ya Madini, ajira 15,341 zamwagwa, manunuzi ya ndani ya nchi yafikia Dola za Marekani bilioni

Read More...

MAFURIKO YAUWA 190 MALAWI

Takriban watu 190 sasa wamethibitishwa kufariki nchini Malawi baada ya Dhoruba ya Mafuriko ya Tropiki Freddy kulikumba eneo

Read More...

Leave a reply:

Your email address will not be published.

Mobile Sliding Menu