Makamu wa Rais amesema serikali haitarudi nyuma kamwe katika mapambano dhidi ya rushwana ufisadi

In Kitaifa

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan , amesema kuwa serikali haitarudi nyuma kamwe katika mapambano dhidi ya rushwa na ufisadi nchini mpaka hapo vitendo hivyo vitakapokoma.

Samia Suluhu  ametoa kauli hiyo wakati anafungua Mkutano wa Kimataifa wa ngazi ya Juu, wenye lengo la kubadilishana uzoefu katika mapambano dhidi ya rushwa katika ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam.

Makamu wa rais ameeleza kuwa vita ya kupambana na vitendo vya rushwa na ufisadi ni kipaumbele cha kwanza ,katika Serikali ya awamu ya Tano na wale wote wanaowezesha, kunufaika na kuhusika na vitendo hivyo wataendelea kuchukuliwa hatua kali za kisheria ili kukomesha vitendo hivyo nchini humo.

Aidha amesema Serikali ya  Awamu Tano chini ya Uongozi Shupavu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli, inaendelea kukaza kamba katika mapambano dhidi ya rushwa ambayo kwa muda mrefu sasa yamechangia kurudisha nyuma, juhudi za Serikali za kuwaletea wananchi maendeleo endelevu.

Amesema Serikali ya Tanzania inalenga kufikia kipato cha kati na kuimarisha uchumi wa viwanda hadi ifikapo mwaka 2025 hivyo malengo hayo yatafanikiwa haraka iwapo tu vitendo vya rushwa vitakomeshwa katika ngazi zote nchini.

 

 

 

Join Our Newsletter!

Get updates, news etc from us. Its simple just put in your email address.

You may also read!

JUMLA YA WATU 2249 VISIWA VYA MULEBA WAPATIWA ELIMU YA UGONJWA WA MARBURG .

Baadhi ya Watalaam wa Afya kutoka Wizara ya Afya wakitoa Elimu katika kisiwa Cha Rushonga kilichopo ndani ya ziwa

Read More...

MAANDALIZI DIRA YA MAENDELEO 2050 YAANZA

SERIKALI  imeanza mchakato Wa kuandaa Dira Mpya ya Maendeleo 2050 ambapo wadau wote katika maeneo yao wametakiwa kushiriki kikamilifu

Read More...

Viwango vya maadili kwa viongoiz yaongezeka.

Imeelezwa kuwa viwango vya uzingatiwaji wa maadili kwa viongozi na watumishi wa umma nchini,vimeongezeka hadi kufikia asilimi 75.9 kwa

Read More...

Leave a reply:

Your email address will not be published.

Mobile Sliding Menu