Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika kongamano la kuwajengea uwezo viongozi wanawake katika kutambua nafasi yao ili kuwawezesha kupata ujasiri wa kuongoza wengine pamoja na kuwaelimisha jinsi ya kujilinda na unyanyasaji wa kijinsia.
Hayo yamesemwa na Mratibu wa Kongamano hilo, Mchungaji Debora Malassy wakati akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana. Pia kongamano hilo litatumika kuwaelimisha wanawake jinsi ya kujikwamua kiuchumi na kutoa elimu ya ukatili wa kijinsia unaotokana na rushwa ya ngono.
Pia amesema kongamano hilo litatumika kumuombea Rais John Magufuli pamoja na taifa kwa ujumla
Ameongeza kuwa kongamano hilo litawakutanisha wanawake kutoka ndani na nje ya nchi mbalimbali ikiwemo Uingereza, Uganda, Congo, Botswana pamoja na Zam
