Makamu wa Rais wa Marekani na naibu Waziri mkuu wa Japan wakubaliana kuweka msukumo wa kidiplomasia na kiuchumi dhidi ya Korea Kaskazini.

Makamu wa Rais wa Marekani Mike Pence na naibu Waziri mkuu wa Japan Taro Aso,wamekubaliana kuweka msukumo wa Kidiplomasia na kiuchumi dhidi ya Korea Kasikazini kuishinikiza kuachana na mpango wake wa silaha za Nyuklia.
Akizungumza mjini Tokyo Japan, Pence amesema Marekani ina amini kuwa njia yenye mafanikio ni mazungumzo ya kimataifa kuishinikiza na kuitenga Korea Kaskazini kutokana na msimamo wake,lakini amesisitiza kuwa njia zote zina uzito wake.
Marekani itaendelea kushirikiana na Japan na washirika wengine katika ukanda na China,kuweka vikwazo vya kidplomasia na kiuchumi dhidi ya Korea Kaskazini,ili iachane na mpango wake wa silaha za nyuklia.Lakini mapendekezo yote yanaendelea kujadiliwa.
Katika mkutano huo Abe amemwambia Pence kuwa Japan inataka kufikia makubaliano kwa njia ya majadiliano.
Marekani kwa sasa imekuwa ikitafutwa uungwaji mkono katika kuikabili Korea Kaskazini.

 

Exit mobile version