Makamu wa rais wa amtembelea Tundu Lissu.

In Kitaifa

Makamu wa rais Mama Samia Suluhu Hassan alimtembelea mbunge wa Singida mashariki nchini Tanzania Tundu Lissu ambaye amelazwa katika hospitali ya Nairobi.

Kulingana na gazeti la The Citizen , makamu huyo alienda hospitalini humo muda mfupi baada ya kuhudhuria kuapishwa kwa rais Uhuru Kenyatta tarehe 28 Novemba.

Bwana Lissu amekuwa akipokea matibabu katika hospitali hiyo tangu mwezi Septemba 7 baada ya kupigwa risasu na watu wasiojulikana katika jaribio la mauaji huko nyumbani kwake mjini Dodoma.

Makamu huyo wa rais ambaye aliandamana na kamishna w atanzania nchini Kenya Dkt. Pindi Chana aliwasili katika hospitali hiyo mwendo wa saa kumi na moja.

Kwa mujibu wa gazeti hilo bi Samia ndio afisa wa ngazi ya juu wa serikali ya Tanzania kumtembelea bwana Lissu miezi mitatu baada ya shambulio.

Bwana Lisuu ambaye pia ni mkuu wa chama cha mawakili nchini Tanzania amekuwa akizozana na serikali ya rais Magufuli na alikamatwa mara sita mwaka huu pekee, akishtumiwa kwa kumtusi kiongozi huyo wa taifa mbali kuharibu usalama wa umma, miongoni mwa mashtaka mengine.

Ndiye kiongozi wa bunge wa upinzani na wakili mkuu wa chama cha Chadema.

Alikamatwa mara ya mwisho mnamo mwezi Agosti baada ya kufichua kwamba ndege ilionunuliwa na kampuni ya ndege ya kitaifa Air Tanzania imekamatwa nchini Canada kutokana na deni la shilingi bilioni 83.

Join Our Newsletter!

Get updates, news etc from us. Its simple just put in your email address.

You may also read!

JUMLA YA WATU 2249 VISIWA VYA MULEBA WAPATIWA ELIMU YA UGONJWA WA MARBURG .

Baadhi ya Watalaam wa Afya kutoka Wizara ya Afya wakitoa Elimu katika kisiwa Cha Rushonga kilichopo ndani ya ziwa

Read More...

MAANDALIZI DIRA YA MAENDELEO 2050 YAANZA

SERIKALI  imeanza mchakato Wa kuandaa Dira Mpya ya Maendeleo 2050 ambapo wadau wote katika maeneo yao wametakiwa kushiriki kikamilifu

Read More...

Viwango vya maadili kwa viongoiz yaongezeka.

Imeelezwa kuwa viwango vya uzingatiwaji wa maadili kwa viongozi na watumishi wa umma nchini,vimeongezeka hadi kufikia asilimi 75.9 kwa

Read More...

Leave a reply:

Your email address will not be published.

Mobile Sliding Menu