Mama akiri kuua Watoto wake wanne.

In Kimataifa


Mwanamke mmoja nchini Kenya Betrice Mwende,
anayeshikiliwa kwa tuhuma za kuwaua watoto wake wanne,
amekiri Mahakamani kuwa ni kweli alifanya tukio hilo na
alilitekeleza kwa kumnyonga mmoja baada ya mwingine na
kwamba alikuwa anajisikia vizuri mno wakati anatenda unyama
huo.


Betrice Mwende mwenye umri wa miaka 41, ambaye pia ni
Mwalimu wa Hisabati, amekiri tuhuma hizo mbele ya Hakimu
Mkaazi wa Mahakama ya Naivasha Yusufu Barasa, na kusema
kuwa alianza kumuua kwa kumnyonga mwanaye mdogo
mwenye umri wa miaka miwili Whitney Nyambura na kisha
kuwaua wengine Melody Warigia (8), Willy Macharia (6) na
Samantha Njeri (4)


Mwende amedai kuwa alitekeleza unyama huo kutokana na
msukumo wa nguvu asizozielewa, huku akimlaumu mmewe
walioachana kwa kusababisha maafa ya wanawe.
Kwa upande wa Mahakama ya Naivasha metoa siku saba zaidi
za mwanamke huyo kuzuiliwa ili aweze kufanyiwa uchunguzi

wa akili, na mwanamke huyo amemwomba kaka yake
kumsaidia kuwazika wanawe, huku akiiomba Mahakama
kumsamehe kwani hakuelewa alichokuwa akifanya.

Join Our Newsletter!

Get updates, news etc from us. Its simple just put in your email address.

You may also read!

Saba washikiliwa kwa tuhuma za mauaji ya hakimu.

Jeshi la Polisi mkoani Mbeya linawashikilia watu saba kwamauaji ya Hakimu Mkazi wa wilaya ya Handeni mkoani TangaJoachim Mwakyolo

Read More...

Ali Reza Akbari ahukumiwa kifo

Iran imemuhukumu kifo afisa mkuu wa zamani wa ulinzi baada kumkuta na hatia kwa mashtaka ya kuifanyia ujasusi Uingereza,

Read More...

Polisi wakamata usafiri uliotumika kuutupa mwili Chiloba

Miongoni mwa waliokamatwa ni watoto wawili huku mshukiwa mkuuJackton Odhiambo akikiri kumuua mwanamitindo huyo kwa usaidizi wawashirika wawili ambao

Read More...

Leave a reply:

Your email address will not be published.

Mobile Sliding Menu