Mama Mkwe wa rafiki yangu ananitaka kimapenzi. Nimemwambia jamaa yangu ushauri wake…

In Mahusiano

Jamaa yangu ameoa binti mmoja mzuri mwaka wa pili sasa, na mimi ndo nilikuwa best man wake so nilihusika vizuri sana

kwenye hiyo ndoa na harusi yao toka mwanzo. katika harakati hizo ndipo Mama mkwe wetu alichukua namba yangu ya simu na tukawa tuna mawasiliano. huyu Mama yeye ameajiriwa Bank flani hapa DSM na aliyeolewa ni mtoto wake wa kwanza. ana watoto wawili tu na mumewe alifariki miaka 6 iliyopita kwa ajali akitokea Bungeni Dodoma alikuwa ni Mwajiriwa Wizara ya fedha.

mwanzoni nlidhani tu kuwa ni ile hali ya kuwa mama wa mjini so hapendelei sana ule umama mkwe wa kijijini au wa kizamani. ukimwona huwez dhani ana miaka 46 anavyojipenda na anavyoonekana kama ni mdada tu wa miaka 30s. na hata ukimwona na mwanaye utadhani ni mdogo wake.so hapendi sana kuwa kama mama na zile heshima za umama.

nilishtuka siku moja aliponambia ameniota..nikamwuliza umeota jambo gani mama… alinambia niite tu flan ili uwe huru kuongea nami.basi kwa shingo upande nikaanza mwita hilo jina. akawa anashindwa kunambia lakini baada ya week akasema ameota tena kama ndoto ya kwanza.alinambia aliota tumekumbatiana.. na alishangazwa why ameota hivyo so akaona kuna kitu hapo. tulichat na sometime anapiga tunaongea. lakini hali imekuwa mbaya coz kuna siku alinambia niende kwake na huko aliamua kabisa kunifanyia vituko kwa nguo alizovaa.alikunywa wine mimi bahati mbaya nlimwambia situmii kilevi chochote alinisihi sana nijaribu nilikataa. akanywa yeye na baadaye akaanza vituko sana na kufikia hatua ya kuja kunikumbatia huku akinikiss. nlimwomba niondoke nikafanikiwa kuondoka.

kesho yake aliniomba msamaha na kusema ni pombe na pia upweke ndiyo uliomufanya awe vile alivyokuwa siku ile.nlimwambi naelewa asiwe na shida. lakini nimeona bado anaonesha mapenzi makubwa kwangu. na anafahamu mimi nimeoa na ninaishi na mke wangu. ilibidi nimwambie jamaa kuwa mama mkwe nadhani ana jambo linamsumbua.ila nikamsihi sana asimwambie mkewe. kwa kushangaa jamaa yangu akanambia ” kama anakuletea hizo we mnanii tu ili akuheshimu” nlishtuka sababu sikutegemea jamaa angesema hivyo. na huyu mama amefikia hatua anasema tu wazi kwangu kuwa anaomba sana angalau awe nami sehemu tukumbatiane tu siku nzima.ana miss sana jambo hilo kwa miaka mi 3 sasa.

nimejaribu sana kumwambia mimi namheshimu sana mke wangu na kuwa hilo jambo halitaleta picha nzuri hata kwa mwanaye akijua maana mwanaye ninaheshimiana naye sana.ila naona kama bado mama mkwe amepania sana. na jamaa yangu hana msaada wowote kwangu zaidi ya kunambia eti mimi nina mlegezea. waswas wangu bintiye asije akajua jambo hili maana ninaheshimiana naye sana.

Join Our Newsletter!

Get updates, news etc from us. Its simple just put in your email address.

You may also read!

Maagizo ya wizara kuhusu mfuko wa maendeleo ya kilimo.

Naibu Waziri Wa Kilimo Anthony Mavunde, amesema serikaliimeanza kutekeleza uanzishwaji wa mfuko wa maendeleo yakilimo utakaosaidia kukabiliana na changamoto

Read More...

TANZIA: WAZIRI MSTAAFU WA KILIMO AFARIKI DUNIA

Aliyewahi kuwa mbunge wa jimbo la Musoma Vijijini na Waziri wa Kilimo na Mifugo Mhe. Herman Kirigini Amefariki Dunia. Akithibitisha

Read More...

Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Professor Makame Mbarawaameliomba Bunge kumuidhinishia kiasi cha Sh Trilioni 3.6ikiwa ni makadirio ya mapato

Read More...

Leave a reply:

Your email address will not be published.

Mobile Sliding Menu