Ghasia na kufyatua risasi ilijitokeza nchini Venezuela, baada ya mamia ya raia walipoandamana mitaani wengine wakimuunga mkono rais Nicolas Maduro, na wengine wakiipinga serikali.
Polisi wa kuzuia ghasia walitumia gesi ya kutoa machozi na risasi za mpira kuwatawanya wapinzani mjini Caracas, ambapo kijana mmoja alipigwa risasi na kupoteza maisha.
Katika Mji wa magharibi mwa nchi hyo San Cristobal, mwanamke mmoja aliuawa mara baada ya maandamano kugeuka vurugu.
