Mamia ya wafanyakazi kutoka katika kikosi cha kupambana na majanga ya moto wanapambana ili kuudhibiti moto mkubwa uliozuka katika msitu mkubwa katikati mwa Ureno, ambao umeua watu sitini mpaka sasa.

In Kimataifa
Mamia ya wafanyakazi kutoka katika kikosi cha kupambana na majanga ya moto wanapambana ili kuudhibiti moto mkubwa uliozuka katika msitu mkubwa katikati mwa Ureno, ambao umeua watu sitini mpaka sasa.
Inaarifiwa kuwa watu wengi walifia katika gari zao wakati walipokuwa katika harakati za kuondoka katika eneo la tukio wilayani Pedrógão Grande.
Akizungumza baada ya kutembelea eneo la tukio, waziri mkuu nchini humo , Antonio Costa, amesema kwamba wazima moto wamekwisha dhibiti mioto zaidi ya miamoja na hamsini nchini mwake.
Waziri Antonio ametangaza siku tatu za maombolezo na kueleza kuwa ni janga kubwa kwa nchi yake, kutoakana na kukabiliwa na majanga ya mioto mikubwa inayozuka katika misitu mikubwa miaka ya karibuni .
Vikosi viwili vya jeshi vimepelekwa katika eneo la tukio ili kuongeza nguvu na kutoa msaada wa dharula.
Umoja wa Ulaya,Ufaransa na Hispania kwa pamoja wamejitolea kutoa msaada wowote utakao hitajika, ikiwemo ndege za kupambana na mioto mikubwa kama hiyo.

Join Our Newsletter!

Get updates, news etc from us. Its simple just put in your email address.

You may also read!

Viwango vya maadili kwa viongoiz yaongezeka.

Imeelezwa kuwa viwango vya uzingatiwaji wa maadili kwa viongozi na watumishi wa umma nchini,vimeongezeka hadi kufikia asilimi 75.9 kwa

Read More...

Watu 193 wawekwa karantini kisa virusi vya Marburg.

Mganga Mkuu wa serikali Dkt Tumaini Nagu,amesema hakuna kisa kipya kilichoongezeka kuhusu vifo vilivyosababishwa na virusi vya Ugonjwa wa

Read More...

SERIKALI YAFANYA UWEKEZAJI MKUBWA KATIKA HUDUMA ZA HALI YA HEWA

SERIKALI kupitia Wizara ya Ujenzi na uchukuzi,isemema kuwa katika kuhakikisha wanakuwa na Taarifa za uhakika za Hali ya hewa

Read More...

Leave a reply:

Your email address will not be published.

Mobile Sliding Menu