Mamilioni ya watu leo watapiga kura kwenye uchaguzi mkuu nchini Uingereza.

In Kimataifa

Mamilioni ya watu leo watapiga kura kwenye uchaguzi mkuu nchini Uingereza.

Shughuli ya upiganji kura itaaza mwendo wa saa moja asubuhii saa za Uingereza wakati zaidi ya vituo 40,000 vitafunguliwa kote nchini.

Jumla ya wabunge 650, watachaguliwa huku takriban watu milioni 46.9 wakiwa wamejiandikisa kupiga kura.

Ni ongezekao kutoka uchaguzi wa mwaka 2015 wakati wapiga kura milioni 46.4 walikuwa wamejiandikisha.

Kura zingine tayari zimepigwa kupitia kwa posta ambayo ilichukua asilimia 16.4 wakati wa uchaguzi wa mwaka 2015.

Vituo vingi vya kupigia kura viko shuleni na katika vituo vya kijamii.

Matokeo ya viti kadha yanatarajiwa kutangazwa ifikapo usiku wa manane huku matokeo ya mwisho yakitarajiwa kutangazwa ifikapo Ijumaa mchana.

 

 

Join Our Newsletter!

Get updates, news etc from us. Its simple just put in your email address.

You may also read!

Wazazi wahimizwa kuzingatia Elimu Mbeya.

Afisa Tarafa wa Sisimba John Mboya amewataka wazazi na walezi kata ya Itagano Jijini Mbeya kuzingatia suala la elimu

Read More...

PROF. NDALICHAKO AKIPONGEZA KIWANDA CHA MBOLEA CHA ITRACOM KWA UTEKELEZAJI SHERIA ZA KAZI

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Prof. Joyce Ndalichako amekipongeza kiwanda

Read More...

WATOTO 109,514 KUPATIWA CHANJO YA MATONE DHIDI YA POLIO WILAYANI NKASI MKOANI RUKWA

Katika utekelezaji wa zoezi la Kampeni ya chanjo ya matone dhidi ya ugonjwa wa  Polio, Halmashauri ya Wilaya ya Nkasi

Read More...

Leave a reply:

Your email address will not be published.

Mobile Sliding Menu