Mamlaka ya hali ya hewa waongelea hali ya mvua.

Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania imekutana na wanahabari leo October 17, 2017 na kueleza juu ya uelekeo wa hali ya hewa hasa uwepo wa mvua ikisema itakuwa nzuri kwa kipindi hiki kwa kuwa na mvua za wastani hadi juu ya wastani.

Hayo yamesemwa na Mkurugenzi wa mamlaka ya hali hewa hapa nchini Dr. Agnes Lawrence Kijazi na kutoa mchangunuo kuhusiana mikoa

Lakini pia Dr. Agnes Lawrence Kijazi ametoa ushauri kutokana na mvua zinazotarajiwa kunyesha na kuwataka wakulima kuandaa mashamba vyema ili kupata mazao pia wananchi kuvuna maji kwa wingi kwa ajili ya matumzi ya baadaye majumbani na pia mashambani.

Exit mobile version