Mamlaka ya hifadhi ya ngorongoro imezindua mradi wa maji uliotumia kiasi cha zaidi ya milioni 231 ikiwa ni utekelezaji wa agizo la waziri mkuu alilolitoa kwa mamlaka hiyo mara alipotembelea la kuwataka wafugaji kutopeleka tena mifugo yao ndani ya kreta.
Aidha mradi huo wenye malambo mawili pamoja na kisima utatumika kwa ajili ya kunyweshea ng’ombe 60 kwa kila lambo moja kwa wakati mmoja huku maji ya kisima yakitumika kwa matumzi ya maji safi na salama kwa jamii inayoishi ndani ya hifadhi hiyo.
Akizindua rasmi mradi huo wa maji uliopo maeneo ya Ndepe katika kata ya Ngorongoro mkuu wa mkoa wa arusha Mrisho Gambo alisema kuwa anaipongeza mamlaka hiyo kwa kutekelezs kwa wakati agizo hilo la waziri mkuu kwani kwa sasa hakuna tena mifugo ambayo inaingia ndani ya kreta .
Alisema kuwa kutokana na upatikanaji wa mradi huo kwa sasa mamlaka hiyo inapaswa kutunga sheria ndogo za kuthibiti mifugo kuingia ndani ya kreta ikiwa ni pamoja na uwekaji alama ili watakaovuka mipaka waweze kuchukuliwa hatua za kisheria kwani kuruhusu mifugo kuingia ndani ya kreta ni uharibifu wa uhifadhi.
Akizungumza katika uzinduzi huo, Mhifadhi mkuu wa hifadhi ya Ngorongoro, Dokta Freddy Manongi alisema kuwa, mradi huo ulianza kujengwa machi 21 mwaka huu na kumalizika April 12 huku ukigharimu kiasi cha shs 231 na 400 ambapo maji yalipatikana kutoka kilometa 11.4 toka chanzo cha maji.
Dk manongi alisema kuwa ni jukumu la mamlaka hiyo kuboresha maisha ya wanaoishi ndani ya mamlaka na hivyo wanaamini upatikanaji wa mradi huo utapunguza changamoto ya mifugo kutrmbea umbali mrefu kwa ajili ya kutafuta maji.
Alidai kuwa mradi huo pia utapunguza malalamiko yaliyokuwa yanatolewa na watalii pindi wa wanapofika ndani ya kreta kwani awali watalii walikuwa wanapunguwa ndani ya kreta kutokana na mifugo
Alisema kuwa kutokana na upatikanaji wa mradi huo kwa sasa mamlaka hiyo inapaswa kutunga sheria ndogo za kuthibiti mifugo kuingia ndani ya kreta ikiwa ni pamoja na uwekaji alama ili watakaovuka mipaka waweze kuchukuliwa hatua za kisheria kwani kuruhusu mifugo kuingia ndani ya kreta ni uharibifu wa uhifadhi.
Mwenyekiti wa baraza la wafugaji Edward Maura alisema kuwa mradi watahakikisha kuwa wanautunza vizuri kwa faida ya mifugo lakini hata kwa matumizi ya binadamu kwani imewaondolea jamii hiyo adha ya kutafuta maji umbali mrefu wa km 12 .
