Mamlaka ya maji safi na usafi wa mazingira jiji la Arusha (AUWSA) yatoa wiki mbili kwa wadaiwa sugu kabla ya hatua kali kuchukuliwa.

Mamlaka ya maji safi na usafi wa mazingira jiji la Arusha (AUWSA) imetoa wiki mbili kwa wateja wote wanaotumia huduma ya maji zikiwemo taasisi za serikali  idara za serikali na watu binafsi kabla ya hatua kali kuchukuliwa ikiwa ni pamoja na kukatiwa huduma ya maji.

Hayo yamesemwa na mwenyekiti wa body ya maji mkoa wa Arusha Doct Job Thomas Laizer na kusema wadaiwa sugu ni pamoja na idara ya mambo ya ndani ambayo ni jeshi la polisi mkoa wa arusha ambayo inadaiwa kiasi cha shs bil.1.2huku hospitali ya mount meru ikidaiwa kiasi cha shs
mil.175.

Doct job amesema fedha hizo zinahitajika kwa ajili yakuendeleza miradi ya maji kwa jiji la arsuha na kutanua huduma za maji katika jiji hili na kuweza kupiga hatua kwa kua mamlaka kwa sasa inatumia fedha zake katika kujiendeleza na si kutegemea fedha kutoka serikalini

Amesema kwa sasa jiji la Arusha linazalisha maji kati ya 30 na 60 elfu mita za ujazo kwa kuwa vyanzo vya sasa haviwezi kuzalisha maji zaidi ya hapo kwani uzalisha wa maji unatagemea na msimu ambapo  msimu wa kiangazi maji hupunguana msimu wa masika maji huongezeka.

Exit mobile version