Klabu ya Manchester imefanikiwa kubadili marufuku ya miaka
miwili kushiriki katika mashindano ya klabu bingwa Ulaya
kuanzia msimu ujao.
Mahakama ya kutatua mizozo ya michezo ilitangaza kwamba
klabu hiyo imeondolewa makosa ya ya kifedha chini ya sheria
ya Fifa siku ya Jumatatu.
Bodi ya kudhibiti matumizi ya klabu za Uefa CFCB ilitoa
marufuku hiyo Februari baada ya City kukiuka sheria ya
Financial Fiar Play FFP kati ya 2012 na 2016.
Faini ya City ya yuro milioni 30 sasa imepunguzwa hadi yuro
milioni 10.
