Maofisa wa Pakistan wamekamata kilo 20 za madawa ya kulevya aina ya heroin katika ndege ya shirika la ndege la nchi hiyo Pia, iliyokuwa inajiandaa kuondoka kuelekea mjini London nchini Uingereza.
Msemaji wa shirika hilo la ndege amesema madawa hayo yalikamatwa baada ya kufanyika ukaguzi katika uwanja wa ndege wa kimataifa mjini Islamabad.
Madawa ya kulevya aina ya heroin yamekamatwa katika ndege za shirika hilo alau mara tatu tangu mwezi Agosti mwaka jana ikiwemo tukio la wiki iliyopita lililotokea katika uwanja wa ndege wa Heathrow mjini London.
