Mara baada ya waziri wa fedha na mipango Dakt. Philip Mpango kuwasilisha bajeti kuu ya serikali kwa mwaka wa fedha 2017/2018 Tgnp mtandao na asasi za kiraia wameisifu bajeti hiyo huku wakiweka bayana baadhi ya mambo yaliyoonekana kuwa na changamoto kadhaa.
Akizungumza mara baada ya kutazama uwasilishwaji wa bajeti hiyo Mkurugenzi mtendaji wa TGNP Mtandao Lilian Liundi, amesema wao kama asasi ya kiraia walikuwa wakitegemea kuona bajeti hiyo ikiwalenga watu na si vitu ,lakini mpango wa miaka mitano wa pili umeingiza mpango huo wa maendeleo ya watu kuwekwa katikati.
Liundi amesema miongoni mwa mambo ambayo hawajafurahishwa nayo ni suala la ushuru wa karatasi, ambalo suala hilo linalenga moja kwa moja katika elimu,pamoja na suala la vifo vya uzazi ambavyo vimeonekana kuongezeka.
