Marekani imetangaza majina ya wanajeshi wake 7 ambao waliuawa wakati meli yao iligongana na ile ya mizigo katika eneo la bahari ya Japan siku ya Jumamosi.
Wanjeshi hao walipatikana katika maneo yaliyokuwa yamefurika maji ndani ya meli hiyo ya kivita ya USS Fitz gerald.
Wanajeshi wengine watatu walijeruhiwa kwenye kisa hicho ambacho kilitokea karibu na mji wa bandari wa Yokosuka.
Wengi wa wanajeshi walikuwa wamelala wakati meli hizo ziligongana. Marekani inasema kuwa inafanya uchunguzi.
Wanajeshi hao waliripotiwa kutoweka baada ya ajali hiyo.
Kamanda wa meli ya kijeshi Joseph P Aucoin aliwaambai waandishi wa habari kuwa ajali hiyo ilisababisha shimo kubwa kwenye meli ya kijeshi.
