Marekani imethibitisha kwamba Korea kaskazini ilifanyia jaribio kombora la masafa marefu, ambalo kulingana na wataalamu wanaamini linaweza kufika Alaska Marekani.
Waziri wa maswala ya kigeni amelitaja jaribio hilo kuwa vitisho vipya kwa Marekani na dunia, na kuonya kwamba Washington haitakubali hatua ya Korea Kaskazini kujihami na nyuklia.
Pyongyang imedai siku ya Jumanne kwamba, ilifanikiwa kulifanyia majaribi kombora lake la masafa marefu ICBM.
Chombo cha habari cha Korea kaskazini KCNA baadaye kilimnukuu Kim jong un akisema kuwa, jaribio hilo ni zawadi kwa Wamerakani siku yao ya uhuru.
