Waziri wa ulinzi wa Marekani Jim Mattis amesema leo kwamba anaimani Marekani inaweza kuondoa wasi wasi wowote wa Uturuki kuhusiana na uamuzi wa kuwapatia silaha wapiganaji wa Kikundi nchini Syria ambao Uturuki inawaona kama magaidi.
Mattis amesema katika mkutano na waandishi habari nchini Lithuania kwamba serikali yake itafanyakazi kwa karibu na Uturuki kusaidia usalama wao katika mpaka wa kusini.
Wakati huo huo wapiganaji wa Kikurdi nchini Syria wamekaribisha tangazo la serikali ya rais Trump kwamba, itawapatia silaha nzito ili kupambana na kundi la Dola la Kiislamu, lakini Uturuki imesema kila silaha itakayotolewa kwa kundi hilo ni kitisho kwa nchi yake.
Mzozo huo unaweza kuzusha mapigano zaidi baina ya washirika hao muhimu wa Marekani katika mapambano dhidi ya kundi la Dola la Kiislamu wakati kundi hilo la Wakurdi wa Syria linajitayarisha kwa operesheni kubwa kuwaondoa wanamgambo wa IS kutoka ngome yao ya mwisho katika mji wa Raqa.
Wakati huo huo Mattis amesema Marekani na NATO ziko tayari kuweka vifaa muhimu vinavyohitajika, kusaidia kuongeza mfumo wa ulinzi katika mataifa ya eneo
