Marekani yaionya vikali Russia endapo itatumia Nyuklia Kuishambulia Ukraine.

In Kimataifa

Marekani imeionya Russia kuhusu kile ilichokiita “matokeo mabaya” ikiwa itaanzisha mashambulizi ya nyuklia dhidi ya Ukraine.

Mshauri wa usalama wa kitaifa wa Rais Joe Biden, Jake Sullivan, alisema Jumapili kwamba utawala wa Biden utachukua hatua za haraka endapo hilo litatokea.

Sullivan, akizungumza kwenye kipindi cha “Wiki Hii” cha ABC, alisema maafisa wa Marekani wamewaambia maafisa wa Russia kwa faragha kwamba Biden “atajibu bila kusita” ikiwa Rais wa Russia Vladimir Putin ataamuru shambulio la nyuklia, lakini hakufafanua jinsi Marekani ingejibu.

Sullivan alisema Marekani “haitajihusisha na mchezo wa maneno kuhusu ulipizaji kisasi” na Russia. Lakini Sullivan, katika mahojiano tofauti, aliambia kipindi cha “Meet The Press” cha NBC kwamba “Russia inaelewa vizuri kile ambacho Marekani ingefanya katika kukabiliana na matumizi ya silaha za nyuklia nchini Ukraine kwa sababu imeshajieleza bayana kuhusu hatua hizo.”

Jibu la Marekani lilikuja baada ya Putin kuashiria uwezekano wa shambulio la nyuklia wiki iliyopita alipowaita wanajeshi 300,000 wa akiba kusaidia kupigana katika uvamizi wake wa miezi saba nchini Ukraine.

Ongezeko hilo la wanajeshi lilikuja baada ya vikwazo dhidi ya Russia, huku wanajeshi wa Kyiv wakitwaa tena maeneo makubwa kaskazini-mashariki mwa Ukraine ambayo Russia ilikuwa imenyakua katika wiki za mwanzo za vita.

Maandamano makubwa ya kupinga kuitishwa kwa jeshi la Putin yamezuka nchini Russia, huku polisi wakiwakamata mamia ya waandamanaji walioshiriki maandamano ya mitaani mjini Moscow na kwingineko.

Join Our Newsletter!

Get updates, news etc from us. Its simple just put in your email address.

You may also read!

Washukiwa 25 wanaodaiwa kupanga njama za mapinduzi wakamatwa Ujerumani

Maelfu ya polisi leo wamefanya msururu wa misako kote Ujerumani wa washukiwa wa siasa kali za mrengo wa kulia

Read More...

Mkuu mpya wa chuo cha Arusha asimikwa.

Chuo kikuu cha Arusha kimemsimika mkuu mpya wa chuohicho wakati wa mahafali ya 16 ambayo yamefanyika chuonihapo.  Mkuu aliyeachia nafasi

Read More...

Naibu Waziri Silinde atoa maagizo mazito Musoma.

Naibu Waziri Ofisi ya Rais TAMISEMI Mhe David Silindeamemuagiza Mkurugenzi wa Halmashauri ya Musoma VijijiniMkoa wa Mara, Msongela Palela

Read More...

Leave a reply:

Your email address will not be published.

Mobile Sliding Menu