Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mhandisi Hamad Masauni, ameagiza kuchukuliwa kwa hatua kali dhidi ya Mkandarasi ambaye ametelekeza ujenzi wa mradi wa Umwagiliaji, kwenye Gereza la Kilimo Idete mkoani Morogoro.
Ametoa agizo hilo baada ya kutembelea gereza hilo kwa ajili ya kujionea mradi huo, ambapo alielezwa na Mkuu wa Magereza Mkoa wa Morogoro Kamishina Msaidizi Mwandamizi wa Magereza Ramadhan Nyamka.
Aidha baada ya kupata maelezo ya mradi huo, Masauni amelitaka Jeshi la Magereza kufanya uchunguzi dhidi ya Mkandarasi huyo, na ikithibitika anamakosa akamatwe na achukuliwe hatua za kisheria.
Mkandarasi huyo ametelekeza mradi huo wenye thamani ya shilingi Bilioni 2.5 tangu mwaka 2016, kitu ambacho kimemfanya Waziri Masauni atoe agizo hilo.
